Chanjo za COVID-19

Chanjo zinatuzuia dhidi ya virusi ambavyo vinasababisha COVID-19. Kila mtu nchini Australia wa umri wa miaka 5 na zaidi anaweza kuweka nafasi kupata chanjo yake ya bure ya COVID-19.

Kuhusu chanjo za COVID-19

Kila mtu nchini Australia wa umri wa miaka 5 na zaidi, na watoto wengine wa umri wa miezi 6 hadi miaka 4, wanastahiki kupata chanjo ya COVID-19.

Pata kliniki na weka nafasi

Chanjo za COVID-19 ni bure kwa kila mtu nchini Australia. Hii inajumuisha watu wasio na kadi ya Medicare, wageni wa ng'ambo, wanafunzi wa kimataifa, wafanyakazi wa kigeni na wanaotafuta hifadhi.

Kupata chanjo kutasaidi kujikinga wewe, na kukinga familia yako na jamii yako dhidi ya COVID-19.

Serikali ya Australia haijalazimisha chanjo na unaweza kuchagua kuacha kuchanjwa dhidi ya COVID-19.

Maagizo mengine ya afya ya umma ya jimbo na wilaya yanaweza kulazimisha chanjo katika hali fulani. Kwa mfano, kwa aina fulani za ajira na kwa baadhi ya shughuli za jamii.

Chanjo ni salama

Chanjo za COVID-19 ni usalama na zinaokoa maisha. Nchini Australia, Therapeutic Goods Administration (TGA) inaendelea kufuatilia kwa karibu usalama wa chanjo ya COVID-19 na athari zake.

Jifunza zaidi kuhusu kila chanjo inayopatikana nchini Australia:

Kama una maswali yoyote au wasiwasi baada ya chanjo, wasiliana na kliniki ya chanjo yako au daktari yako.

Nani anapaswa kupata chanjo

Kila mtu wa umri wa miaka 5 na zaidi achanjwe dhidi ya COVID-19.

Ili kupata kinga bora kuzuia kuwa mgonjwa sana au kufariki kutokana na COVID-19, unapaswa kupata chanjo zote zinazopendekezwa kwa umri wako na mahitaji yako ya kiafya.

Watoto wengine wa umri wa miezi 6 hadi miaka 4 wanastahiki kupata chanjo ya COVID-19 ikiwa:

 • wana kingamwili dhaifu sana
 • wana ulemavu, au
 • wana hali ngumu na/au nyingi za kiafya zinazoongeza hatari yao ya kuugua COVID-19 kali.

Watoto wa umri wa miezi 6 hadi miaka 4 wanapaswa kupata:

 • vipimo viwili vya msingi vya chanjo ya COVID-19
 • kipimo cha tatu cha msingi ikiwa wana kingamwili dhaifu sana.

Watoto wa umri wa miaka 5 hadi 17 wanapaswa kupata:

 • vipimo viwili vya msingi vya chanjo ya COVID-19
 • kipimo cha tatu cha msingi ikiwa wana kingamwili dhaifu sana
 • kipimo cha nyongeza ikiwa:
  • wana kingamwili dhaifu sana
  • wana ulemavu
  • wana hali ngumu na/au nyingi za kiafya zinazoongeza hatari yao ya kuugua COVID-19 kali
  • imekuwa muda wa miezi 6 tangu kipimo kilichopita au maambukizo ya COVID-19 yaliyothibitishwa.

Daktari yako anaweza kukusaidia kuamua kama mtoto wako anapaswa kupokea kipimo cha nyongeza.

Kila mtu wa umri wa miaka 18 au zaidi anapaswa kupata:

 • vipimo viwili vya msingi vya chanjo ya COVID-19
 • kipimo cha tatu cha msingi ikiwa wana kingamwili dhaifu sana

Kila mtu wa umri wa miaka 18 na zaidi anaweza kufikiria kupata kipimo cha nyongeza kama imekuwa muda wa miezi 6 tangu kipimo chake kilichopita au maambukizo ya COVID-19 yaliothibitishwa.

Jifunza zaidi kuhusu ushauri wa chanjo ya nyongeza ya COVID-19.

Watoto

Data za usalama wa chanjo za COVID-19 kutoka AusVaxSafety huonyesha kuwa watoto wa umri wa miaka 5 hadi 15 huripoti madhara machache katika siku zinazofuata chanjo yao ya COVID-19 kuliko wale katika majaribo ya kimatibabu.

Hakuna uthibitisho kuwa chanjo za COVID-19 husababisha utasa wa baadaye katika watoto.

Jifunza zaidi kuhusu chanjo za COVID-19 kwa watoto na vijana.

Wajawazito au wanawake wanaonyonyesha

Chanjo za COVID-19 ni salama kama wewe ni mjamzito, ukinyonyesha, au ukipanga kupata mimba. Unaweza kupata chanjo katika hatua yoyote ya ujauzito.

Jifunza zaidi kuhusu ujauzito, kunyonyesha, na chanjo za COVID-19.

Watu wenye ulemavu

Watu wenye ulemavu wana hatari kubwa ya ugonjwa mbaya kutokana na COVID-19 na wanapaswa kuchanjwa.

Ikiwa unataka msaada au usaidizi zaidi, unaweza kupiga simu kwa Disability Gateway Helpline kwa 1800 643 787. Wanaweza kuweka nafasi kwa ajili yako.

Ikiwa unahitaji mkalimani, piga simu kwa Translating and Interpreting Service 131 450 na umwombe apigie simu kwa Disability Gateway.

Watu walio na shida za kiafya zilizopo

Watu walio na shida za kiafya zilizopo zina hatari kubwa ya kuugua sana kutokana na COVID-19 na wanapaswa kuchanjwa.

Zungumza na mtoaji wako wa utunzaji wa afya wa kila mara kuhusu chanjo bora kwa hali yako.

Kuchanjwa wapi

Unaweza kupata chanjo ya COVID-19 kwa:

 • kliniki za chanjo za Commonwealth
 • madaktari wa mtaa wanaoshiriki
 • Huduma za Afya Zinazodhibitiwa na Jumuiya za Watu Asili
 • kliniki za chanjo za jimbo na wilaya, na
 • maduka ya dawa yanayoshiriki.

Madaktari wa mtaani hawaruhusiwi kukutozwa kwa chanjo.

Ili kupata kliniki ya karibu kwako na kupanga miadi kwa chanjo yako, tumia Kitafutaji cha Kliniki ya Chanjo.

Ikiwa unahitaji ukalimani wa simu au kwa papo hapo katika miadi yako ya chanjo, pigia simu kwa Huduma ya Utafsiri na Ukalimani kwa 131 450.

EVA, inayojulikana pia kama Easy Vaccine Access (Upatikanaji Rahisi wa Chanjo), ni huduma ya kukusaidia kupanga miadi ya chanjo ya COVID-19 kupitia simu katika lugha yako. EVA hufanya kazi kuanzia saa1 asubuhi (7am) hadi saa4 asubuhi (10pm) (AEST), siku 7 kwa wiki. Jifunza zaidi kuhusu EVA.

Ikiwa huna kadi ya Medicare

Ikiwa huna kadi ya Medicare, unaweza kupata chanjo yako ya bure kutoka maduka ya dawa ya jamii na kiliniki za chanjo za jimbo au wilaya (zinapoendelea kufanya kazi)

Kabla ya chanjo yako ya COVID-19

Ikiwa hujafanya tayari, panga miadi.

Pata kliniki na weka nafasi

Ikiwa una kadi ya Medicare, hakikisha habari yako ni ya sasa hivi;

Unaweza kuulizwa kujaza fomu ya idhini kabla ya miadi yako, au kama unafanya amuzi ya chanjo kwa ajili ya mtu mwingine.

Soma fomu ya idhini.

Soma fomu ya maelezo na idhini kwa watoto wa umri wa miake 5 hadi 11.

Baada ya chanjo yako ya COVID-19

Utafuatiliwa kwa angalau dakika 15 baada ya chanjo yako iwapo mmenyuko wa nadra wa mzio ukitokea. Mtu anayekupa chanjo amefunzwa kushughulikia athari za haraka. 

Kwa kawaida madhara kutokana na chanjo za COVID-19 ni madogo na huisha katika siku 1 au 2. Athari ya kawaida ni pamoja na:

 • mkono kuumwa mahali ambapo sindano ilipoingia
 • uchovu
 • kichwa kuuma
 • maumivu ya misuli
 • homa na baridi.

Kama dawa au chanjo yoyote, kunaweza kuwa madhara adimu au yasiyojulikana. Ikiwa unafikiri unapata madhara mabaya wasiliana na mtaalamu wako wa utunzaji wa afya, au National Coronavirus Helpline (Simu ya Msaada ya Kitaifa ya Virusi vya Korona).

1800 020 080

Iwapo unahitaji mkalimani, pigia simu kwa National Coronavirus Helpline na chagua chaguo la 8.

Uthibitisho wa chanjo

Unaweza kupata uthibitisho wa chanjo yako ya COVID-19 kwa kupata Taarifa ya Historia ya Kuchanjwa.

Unaweza kupata Taarifa yako ya Historia ya Kuchanjwa:

Ikiwa huna kadi ya Medicare, au huna upatikanaji kwa akaunti ya myGov, unaweza kupata Taarifa yako ya Historia ya Chanjo kwa:

 • kuomba mtoaji wa chanjo yako achapishe nakala kwa ajili yako; au
 • kupigia simu kwenye simu ya maswali ya Rejesta ya Chanjo ya Australia kwa 1800 653 809 (saa2 asubuhi [8 am] hadi saa11 jioni [5 pm] Jumatatu [Monday] hadi Ijumaa [Friday] AEST) na kuwaomba watuma taarifa kwako kwa posta. Inaweza kuchukua hadi siku 14 kufikia kwa posta.

Kwa habari zaidi kuhusu jinsi ya kupata uthibitisho wa chanjo zako za COVID-19, angalia kwa tovuti ya Services Australia.

Unaweza kwenda wapi kupata maarifa ya kuaminika

Ni muhimu kuendelea kufahamu kuhusu COVID-19 na mradi wa chanjo ya COVID-19 kupitia vyanzo vya kuaminika na rasmi.

Majibu ya maswali ya kawaida kuhusu chanjo za COVID-19 yanapatikana katika lugha 63.

Kifurushi cha maelezo kilicho na nyenzo za lugha kuhusu chanjo za COVID-19 kinapatikana.

Soma habari kuhusu COVID-19 katika lugha yako.

Nyenzo

Tazama habari za chanjo ya COVID-19 zaidi zilizotafsiriwa.

Last updated:

Help us improve health.gov.au

If you would like a response please use the enquiries form instead.