Kuhusu chanjo za COVID-19

Kila mtu katika Australia wa umri wa miaka 5 na zaidi anaweza kupanga miadi yake ya chanjo sasa.

Pata kliniki na weka nafasi

Chanjo za COVID-19 ni bure kwa kila mtu nchini Australia. Hii inajumuisha watu wasio na kadi ya Medicare, wageni wa ng'ambo, wanafunzi wa kimataifa, wafanyakazi wa kigeni na wanaotafuta hifadhi. Kupata chanjo kutasaidi kujizuia wewe, na kuzuia familia yako na jamii yako kutoka COVID-19.

Serikali ya Australia hajafanya chanjo kuwa lazima na unaweza kuchagua kutopata chanjo kuzuia COVID-19

Maagizo mengine ya afya ya umma ya jimbo na wilaya yanaweza kulazimisha katika hali fulani. Kwa mfano, kwa aina fulani za ajira na kwa baadhi ya shughuli za jamii.

Chanjo ni salama

Chanjo za COVID-19 ni salama na zinaokoa maisha. Nchini Australia, Therapeutic Goods Administration (TGA) inaendelea kufuatilia kwa karibu usalama wa chanjo ya COVID-19 na athari zake.

Jifunza zaidi juu ya kila chanjo inayopatikana nchini Australia:

Chanjo za COVID-19 hufundisha mwili wako kuviondoa virusi ikiwa unakaribiana na hivi.

Kama una maswali yoyote au wasiwasi baada ya chanjo, wasiliana na kliniki ya chanjo yako au daktari yako.

Jifunza zaidi kuhusu unachotarajia baada ya chanjo yako.

Nani anapaswa kupata chanjo

Kila mtu wa umri wa miaka 5 na zaidi anapaswa kupata chanjo dhidi ya COVID-19.

Kupata chanjo ya COVID-19 kunakuzuia dhidi ya kuwa mgonjwa sana au kufarikia kutokana na COVID-19.

Kupata chanjo pia kunasaidia kuzuia watu wa karibu kwako kwa kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi.

Ili kuzingatiwa kuwa ya kisasa na chanjo zako za COVID-19, unapaswa kulikuwa umepata dozi zote zilizopendekezwa kwa umri wako na mahitaji ya afya.

Kuanzia tarehe 5 Septemba 2022, watoto wengine wa umri wa miezi 6 hadi miaka 4 ambao wana kingamwili dhaifu sana, wana ulemavu, au wana hali ngumu na/au nyingi za kiafya zinazoongeza hatari zao za COVID-19 kali watastahiki kwa chanjo ya COVID-19.

Kuweka nafasi kutapatikana karibu. Tafadhali usipige simu daktari wako kupanga miadi naye. Tutakujulisha wakati kuweka nafasi kunapofungua na jinsi ya kupanga miadi.

Watoto wa umri wa miezi 6 hadi miaka 4 wanapaswa kupata:

 • dozi za msingi ya 1 na 2 za chanjo ya COVID-19
 • dozi ya msingi ya 3 ikiwa wana mfumo wa kinga dhaifu sana.

Watoto wa umri wa miaka 5 hadi 11 wanapaswa kupata:

 • dozi za msingi ya 1 na 2 Za chanjo ya COVID-19
 • dozi ya msingi ya 3 ikiwa ana mfumo wa kinga dhaifu sana.

Watoto wa umri wa miaka 12 hadi 15 wanapaswa kupata:

 • dozi ya msingi ya 1 na 2 ya chanjo ya COVID-19
 • dozi ya msingi ya 3 ikiwa wana kingamwili dhaifu sana.
 • dozi ya nyongeza ya chanjo ya COVID-19 ikiwa wale:
  • wana kingamwili dhaifu sana
  • wana ulemavu wenye mahitaji muhimu au magumu ya kiafya
  • wana hali ngumu na/au nyingi za kiafya zinazoongeza hatari ya COVID-19 kali.

Zungumza na daktari wako ikiwa huna uhakika kama mtoto wako anapaswa kupokea chanjo ya nyongeza.

Kila mtu wa umri wa miaka 16 au zaidi anapaswa kupata:

 • dozi ya msingi ya 1 na 2 ya chanjo ya COVID-19
 • dozi ya msingi ya 3 ikiwa wana mfumo wa kinga dhaifu sana
 • dozi ya nyongeza cha chanjo ya COVID-19.

Vipimo vya vinne

Kipimo ziada cha nyongeza, au kipimo cha nne, cha chanjo ya COVID-19 kinapendekezwa kwa watu wenye hatari zilizoongezeka ya ugonjwa mbaya, kupewa miezi 3 baada ya kipimo chao cha kwanza cha nyongeza.

Hiki kitakuwa kipimo cha tano kwa watu ambao wana kingamwili dhaifu sana, wana hali ya kimatibabu au ulemavu.

Unapaswa kupata kipimo cha nne ikiwa wewe:

 • una umri wa miaka 50 au zaidi
 • ni mkazi wa kituo cha huduma ya wazee au ya wenye ulemavu
 • una kingamwili dhaifu sana (hiki kitakuwa kipimo cha tano)
 • ni mtu wa Aboriginal au Torres Strait Islander na una umri wa miaka 50 au zaidi
 • una umri wa miaka 16 au zaidi na pia hali ya matibabu ambayo inaongezeka hatari ya ugonjwa mbaya wa COVID-19
 • una umri wa miaka 16 au zaidi mwenye ulemavu au mahitaji magumu ya afya.

Watu wa umri wa miaka 30 hadi 49 wanaweza kupokea kipimo cha nne wakichagua.

Zungumza na daktari wako ikiwa huna hakika ikiwa unapaswa kupokea kipimo cha nne cha nyongeza.

Ikiwa umepimwa chanya una COVID-19 inapendekezwa usubiri miezi 3 baada ya maambukizi ya COVID-19 kabla hujapokea kipimo chako kijacho cha chanjo ya COVID-19.

Watu ambao waliugua COVID-19 baada ya kipimo chao cha nyongeza wanapaswa pia kusubiri angalau miezi 3 kabla ya kupata kipimo cha nne.

Ni muhimu kuendelea kusasisha na chanjo zako za COVID-19. Watu tofauti wanaweza kuhitaji chanjo tofauti za COVID-19 katika nyakati tofauti. Zungumza na mtoa huduma yako ya afya ili kujua unachohitaji kufanya wewe na familia yako ili kusasisha.

Watoto

Chanjo za COVID-19 ni salama kwa watoto.

Chanjo kwa watoto wanaweza kuwazuia kuambukiza virusi kwa wadogo wao, bibi na babu wao, na jumuiya.

Jifunza zaidi kuhusu Chanjo za COVID-19 kwa watoto na vijana.

Wajawazito au wanawake wanaonyonyesha

Chanjo za COVID-19 ni salama ikiwa wewe ni mjamzito, unanyonyesha, au kupanga ujauzito. Unaweza kupokea chanjo katika hatua yoyote ya ujauzito.

Jifunza zaidi kuhusu ujauzito, kunyonyesha, na chanjo za COVID-19.

Watu wenye ulemavu

Watu wenye ulemavu wanakabiliwa na hatari kubwa ya ugonjwa mbaya kutoka COVID-19 na wanapaswa kuchanjwa.

Ikiwa unataka usaidizi au msaada, unaweza kupiga simu kwa Disability Gateway Helpline kwenye 1800 643 787. Wanaweza kuweka nafasi kwa ajili yako.

 Ikiwa unahitaji mkalimani, piga simu kwa Translating and Interpreting Service 131 450 na umwombe kupiga simu kwa Disability Gateway.

Watu walio na shida za kiafya zilizopo

Watu walio na shida za kiafya zilizopo wako hatari kubwa wa ugonjwa mkubwa kutokana na COVID-19 na wanapaswa kuchanjwa.

Zungumza na mtoa huduma yako ya kawaida ya afya kuhusu chanjo bora kwa hali yako.

Kuchanjwa wapi

Unaweza kupata chanjo ya COVID-19 kwa:

 • kliniki za chanjo za Commonwealth
 • madaktari wa mtaa wanaoshiriki
 • Aboriginal Controlled Community Health Services
 • kliniki za chanjo za jimbo na wilaya, na
 • maduka ya dawa yanayoshiriki.

Madaktari wa mtaani hawaruhusiwi kukutozwa kwa chanjo.

Ili kupata kliniki ya karibu kwako na kupanga miadi kwa chanjo yako, tumia Vaccine Clinic Finder (Kitafuta cha Kliniki ya Chanjo). Ikiwa unahitaji ukalimani wa simu au kwa papo hapo katika miadi yako ya chanjo, pigia simu kwa Huduma ya Utafsiri na Ukalimani kwa 131 450.

Ikiwa huna kadi ya Medicare

Ikiwa huna kadi ya Medicare, unaweza kupata chanjo yako ya bure katika:

 • kliniki za chanjo za Commonwealth
 • kliniki za chanjo za jimbo au wilaya
 • maduka ya dawa yanayoshiriki.

‘Hey Eva’ – Ufikiaji Rahisi wa Chanjo

EVA, ni huduma rahisi ya kupiga simu tena kusaidia watu kuweka nafasi ya chanjo ya COVID-19. EVA huendesha kutoka saa 1 asubuhi hadi saa 4 usiku (7am-10pm) (AEST), siku 7 kwa wiki.

Wakati unapotuma ujumbe kwa EVA utapokea jibu kuuliza kwa:

 • jina lako
 • lugha unayopendelea
 • tarehe na saa unayopendelea
 • nambari nzuri yako ya simu kwa kupata simu ya jibu.

Mwendeshaji simu aliyefunzwa kutoka kwenye National Coronavirus Helpline atakupigia simu tena kwa wakati uliopangwa ili kusaidia kuweka nafasi ya kuchanjwa kwa COVID-19.

EVA hutoa habari na ushauri kuhusu chanjo za COVID-19 na husaidia na:

 • kutoa habari na ushauri kuhusu chanjo za COVID-19
 • kukusaidia kupata kliniki ya kuingia kwa miguu
 • kukusaidia kupata miadi inayofaa ya chanjo
 • kukuunganisha na usaidizi wa ukalimani wa bure.

Kupata usaidizi wa kuweka nafasi kwa chanjo ya COVID-19, SMS ‘Hey EVA’ kwa huduma za EVA za kukupiga simu kujibu kwenye 0481 611 382. EVA huendesha kutoka saa 1 asubuhi hadi saa 4 usiku (7am-10pm) (AEST), siku 7 kwa wiki.

Kabla ya chanjo yako ya COVID-19

Ikiwa hujafanya tayari, panga miadi.

Pata kliniki na weka nafasi

Ikiwa una kadi ya Medicare, kagua habari zako ni za sasa:

Unaweza kuulizwa kujaza fomu ya idhini kabla ya miadi yako, au kama unafanya amuzi ya chanjo kwa ajili ya mtu mwingine.

Soma fomu ya idhini.

Soma fomu ya maelezo na idhini kwa watoto wa umri wa miaka 5 hadi 11.

Baada ya chanjo yako ya COVID-19

Utafuatiliwa kwa angalau dakika 15 baada ya chanjo yako katika kesi ya mmenyuko wa nadra wa mzio. Mtu yule anayekupa chanjo amefunzwa kutunza mmenyuko wa mara moja.

Kwa kawaida athari kutoka chanjo za COVID-19 ni ndogo na huondoka katika siku 1 au 2. Athari ya kawaida ni pamoja na:

 • mkono kuumiwa mahali ambapo sindano ilipoingia
 • uchovu
 • kichwa kuumia
 • maumivu ya misuli
 • homa na baridi.

Kama dawa lolote au chanjo yoyote, kunaweza kuwa athari za nadra au athari zisizojulikana. Ikiwa unafikiri una athari kubwa wasiliana na mtaalamu wako wa afya, au National Coronavirus Helpline.

1800 020 080

Ikiwa unahitaji mkalimani , piga simu kwa National Coronavirus Helpline na chagua chaguo la 8.

Uthibitisho wa chanjo

Unaweza kupata uthibitisho wa chanjo yako ya COVID-19 kwa kupata Taarifa yako ya Historia ya Chanjo.

Unaweza kupata Taarifa yako ya Historia ya Chanjo:

Ikiwa huna kadi ya Medicare, au huna upatikanaji kwa akaunti ya myGov, unaweza kupata Taarifa ya Historia ya Chanjo yako kwa:

 • kuomba mtoaji wa chanjo yako kuchapisha nakala kwa ajili yako; au
 • kupiga simu ya laini ya maswali ya Australian Immunisation Register kwenye 1800 653 809 (saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni Jumatatu hadi Ijumaa AEST) (8 am – 5 pm) na kuwaomba kutuma taarifa yako kwako katika posta. Inaweza kuchukua hadi siku 14 kufikia kwa posta.

Kwa habari zaidi kuhusu jinsi ya kupata uthibitisho wa chanjo zako za COVID-19, angalia kwa tovuti ya Services Australia.

Unaweza kwenda wapi kwa maelezo ya kuaminika

Ni muhimu kuendelea kufahamishwa kuhusu COVID-19 na mradi wa chanjo ya COVID-19 kupitia vyanzo vya kuaminika na rasmi.

Majibu kwa maswali ya kawaida kuhusu chanjo za COVID-19 yanapatikana katika lugha 63.

Kifurushi cha taarifa kilicho na nyenzo za lugha kuhusu chanjo za COVID-19 kinapatikana.

Soma habari kuhusu COVID-19 katika lugha yako.

Rasilimali

Language: 
Swahili - Kiswahili
Last updated: 
21 September 2022