The government is now operating in accordance with the Guidance on Caretaker Conventions, pending the outcome of the 2025 federal election.

Kujiandikisha katika MyMedicare

Unaweza kujiandikisha katika MyMedicare kwa kutumia Akaunti yako ya Medicare Mtandaoni au Programu ya Simu ya Express Plus Medicare, au kwa kujaza fomu utakapotembelea Daktari wako.

1:41

MyMedicare ni njia mpya ya kurasimisha uhusiano kati ya wagonjwa na watoa huduma zao za afya.

Wakati mgonjwa na mtoaji wa huduma wanayempendelea wote wamesajiliwa katika MyMedicare, ufadhili wa ziada wa serikali unapatikana ili kuwasaidia kutoa zaidi ya utunzaji na huduma zinazolengwa na wagonjwa wao.

Hatua ya kwanza ni kuangalia kama unastahiki. Unaweza kujiandikisha katika MyMedicare ikiwa:

  • Una kadi ya Medicare au Kadi ya Idara ya Mambo ya Watu Wazee, na
  • umekuwa na miadi miwili ya ana kwa ana daktari huyo huyo katika miezi 24 iliyopita - au miadi moja ikiwa unaishi katika eneo la mbali, na
  • Daktari wakowako unayopendelea au huduma ya afya inayostahiki tayari imesajiliwa katika MyMedicare.

Unaweza kujiandikisha katika MyMedicare kwa kutumia Akaunti yako ya Medicare Mtandaoni au Programu ya Simu ya Express Plus Medicare, au kwa kujaza fomu utakapotembelea Daktari wako.

Unapojiandikisha katika MyMedicare, maelezo yako ya kibinafsi yatawekwa salama na faragha yako itadumishwa

Zungumza na daktari wako (GP) au mtaalamu wa afya kuhusu kujiandikisha katika MyMedicare. Kwa habari zaidi kwa Kiswahili, tembelea health.gov.au/mymedicare.

Video type:
Advertisement
Publication date:
Date last updated:
Part of a collection:

Help us improve health.gov.au

If you would like a response please use the enquiries form instead.