Safari za ndani za nchini Australia
Angalia tovuti za idara za afya za mtaa ili kupata habari kuhusu kusafiri kwa:
Kusafiri nje
COVID-19 huendelea kuwa hatari ya afya nchini Australia na nje ya nchi. Tunashauri kwa nguvu kuvaa maski na kuchanjwa wakati unaposafiri nje ya nchi. Unapaswa kufanya usafi mzuri wa kukohoa na kuosha mikono, na kukaa mbali na wengine inapowezekana.
Baadhi ya nchi, mashirikia ya ndege na waendeshaji wa meli wanaweza kuwa na mahitaji ya COVID-19 ya usafiri wa. Haya yanaweza kujumuisha jibu la kipimo kabla ya kuondoka pale wakati wa check-in kabla ya kuingia ndege au meli yako. Angalia mahitaji ya kuingia ya yote mbili:
-
nchi ambayo unasafiri kwenda, au kuipitia
-
mahitaji ya mwendeshaji wa ndege au meli.
Nyenzo:
Waaustralia wanaorudi nyumbani
Mipaka ya nchi Australia ni wazi, na hakuna mahitaji ya Australian Government:
- kutoa uthibitisho wa kipimo hasi hakuna COVID-19 wakati wa kuasili Australia
- kutoa uthibitisho wa chanjo za COVID-19
- kuvaa maski, ingawa kufanya hivi kunatiwa moyo.
Bima ya usafiri
Bima ya usafiri ni muhimu ikiwa unaugua COVID-19 nje ya nchi. Hakikisha bima yako inajumuisha:
- mahali pa kusafiria
- majumuisho kwa COVID-19
- nyongeza zingine kama bima maalum ya kusafiri kwenye meli.
Mahali pengine pa safari pia panahitaji wasafiri kuwa na bima ya usafiri kama sharti la kuingia.
Usafiri wa meli za abiria
Wasiliana na mtoa huduma wako wa usafiri wa meli kwa mahitaji ya kisasa ya usafiri kwa meli na unakoenda.
Kuchanjwa
Hakuna sharti la Australian Government kwa wasafiri kuchanjwa kwenye meli ya abiria. Hata hivyo, tunapendekeza:
- chanjo ya COVID-19, kwa sababu uko kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata ugonjwa mbaya na COVID-19 ndefu ikiwa hujachanjwa
- kufikiria tena safari yako kwenye meli za baharini ikiwa hujachanjwa.
Milipuko kwenye meli ya abiria
Meli za abiria zina hatari kubwa zaidi kueneza magonjwa ikilinganishwa na aina nyingine za usafiri. COVID-19, mafua na magonjwa mengine ya kuambukiza huenea kwa urahisi kati ya watu wanaoishi na kushirikiana katika maeneo ya karibu.
Ikiwa mlipuko wa COVID-19 ukitokea kwenye meli yako, unaweza kuhitaji:
- kujitenga karantini kwenye meli
- kushuka na kufuata sheria za eneo la jimbo au wilaya au nchi uliopo.
Kabla ya kusafiri, angalia Ushauri wa Smartraveller kuhusu meli za baharini. Wasiliana na wakala wako wa usafiri au mwendeshaji wa meli kwa habari maalum juu ya itifaki zao za salama za COVID-19.
Serikali za majimbo na wilaya hutengeneza na kusasisha itifaki za afya za uendeshaji zinazosaidia usafiri wa baharini nchini Australia.
Itifaki za tasnia ya meli za kusafiri pia husaidia kupunguza hatari ya maambukizi ya COVID-19 kwenye meli za abiria, ikiwa ni pamoja na:
- mahitaji ya chanjo kwa abiria
- mipango ya kudhibiti milipuko
- mipango ya usalama ya COVID-19.
Wasafiri wa kimataifa kwenda nchini Australia
Mipaka ya nchi Australia ni wazi, na hakuna mahitaji ya Australian Government:
- kutoa uthibitisho wa kipimo hasi hakuna COVID-19 wakati wa kuasili Australia
- kutoa uthibitisho wa chanjo za COVID-19
- kuvaa maski, ingawa kufanya hivi kunatiwa moyo.
Pata maelezo zaidi kuhusu kuingia na kuondoka nchini Australia.