Halo, jina langu ni Sankeita na mimi ni muuguzi.
Ninaenda kueleza jinsi chanjo za COVID-19 zinafanya kazi.
Chanjo hudungwa mwilini mwako.
Haziondoi chochote kutoka mwilini
mwako na hazibadilishi jeni zako au DNA.
Chanjo za COVID-19 hufundisha mwili wako kutambua
na kupambana na virusi vya COVID-19. Hazina COVID-19,
na huwezi kupata COVID-19 kutoka kwenye chanjo.
Madhara kidogo, kama maumivu ya kichwa au maumivu ya
misuli, maana chanjo inafanya kazi.
Chanjo za COVID-19 husaidia kuzuia magonjwa
hatari na kifo. Kila mtu anaweza kufanya
sehemu yake kulinda familia na jamii yao kwa kupata chanjo.
Kwa habari zaidi juu ya chanjo za COVID-19 angalia
health.gov.au/covid19-vaccines au piga simu kwa
Msaada wa Kitaifa wa Coronavirus kwenye 1800 020 080.
Huduma ya kutafsiri na ukalimani piga simu 131 450.